Wataalam wa masuala ya anga wamefanikiwa kurekebisha kifaa kinachotunza kumbukumbu ya mwenendo wa ndege cha EgyptAir iliyoanguka mwezi uliopita na kuua watu 66 waliokuwamo ndani yake.
Hatua hiyo inawapa nafasi wachunguzi hao kuweza kuzitafakari na kuzifuatialia taarifa zitakazobainisha ni kwanini ndege hiyo ilianguka mashariki mwa bahari ya Mediterranian. Taarifa rasmi kuhusiana na uchunguzi huo zinasema kuwa kazi ya kusikiliza na kuzifuatilia sauti hizo itafanyika ndani ya saa chache zijazo. Kisanduku hicho cha mawasiliano kimefikishwa mjini Paris Ufaransa jana jumatatu kutoka Cairo Misri ambapo kimepelekwa huko ili kuondoa tabaka za chumvi zilizokizunguka chombo hicho. Hata hivyo kinatarajiwa kurejeshwa katika maabara za mjini Cairo kwa uchunguzi zaidi baada ya marekebisho yote kukamilika. Mapema wanasheria nchini Ufaransa walifungua kesi ya mauaji dhidi ya ajali hiyo kwa madai kuwa ilitokana na hujuma. Wanasema hakuna uthibitisho wowote kuwa ajali hiyo ilitokana na ugaidi.
Post a Comment