0

Timu za Azam na Yanga vitashuka katika dimba la taifa Dar es salaam hapo kesho katika mchezo wa fainali.
Mchezo huu ni wa fainali ya michuano ya kombe la shirikisho ambapo timu hizi mbili zitakuwa zikiwania kikombe na nafasi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Mwamuzi mahiri nchini, Israel Mujuni Nkongo ametuliwa kuchezesha mchezo huu akisaidiwa na Ferdinand Chancha wa Mwanza na Soud Lila na mwamuzi wa akiba atakua ni Frank Salaam huku Kamisaa wa mchezo huo anatakuwa Juma Mgunda.
Fainali ya michuano hii inakuja baada ya timu 64 za Ligi Kuu Tanzania bara,Ligi daraja la Kwanza na ligi daraja la Pili kuchuana na kubakia timu hizi mbili.

Post a Comment

 
Top