0
Watu wengi duniani, hasa vijana, wamegeuzwa watumwa na simu za mkononi na huwa vigumu sana kwao kuweka simu zao chini.
Hili hufanyika hata wanapotembea barabarani na wataalamu wanaonya kwamba hilo limechangia ongezeko la ajali barabarani katika miji mingi.
Si ajabu kwamba katika mji wa Augsburg, Ujerumani wasimamizi wa baraza la jiji wameanzisha mfumo mpya wa kuweka taa za barabarani. Badala ya kuwekwa kwenye milingoti, taa hizo zinawekwa chini ili watu waweze kujua taa zikibadilika bila kuinua vichwa vyao.
Tatizo hilo la watu kutumia sana simu kiasi cha kutotaka kujishughulisha na mambo mengine limepelekea kubuniwa kwa msamiati mpya ambapo waraibu wa hilo wanaitwa Masmombi.
Image copyrightAP
Jina hili limetokana na jina zombi ambalo hutumiwa sana kueleza viumbe ambao hutembea bila kuwa na hiari na huwa hawazungumzi lolote. Tamaduni nyingi huamini kwamba mazombi hudhibitiwa na nguvu za kishirikina na sana huwa na miili ya watu waliofariki kisha wakafufuliwa kwa nguvu hizo za kishirikina.
Dhana hii ya zombi imeunganishwa na jina la simu za kisasa ambazo kwa Kiingereza hujulikana kama smartphone.
Tumewauliza baadhi yenu iwapo mmekabiliwa na tatizo hili la kutumia sana simu na wengi katika ukurasa wetu wa Facebook na katika Instagram wanakubali kwamba hili ni tatizo kubwa.
Keisi Ahuura kutoka Entebbe Uganda amesema: "Kwa kweli Mimi ni #smombi wa daraja la juu. Mda mwingi zaidhi nakuwa kwa net sio kupiga simu.”
Said Mahseen naye anasema hawezi kukaa bila simu mkononi.
"Sijajaribu kupunguza sababu napenda sana kutumia simu, naona raha sana siwezi kukaa bila ya simu mkononi,” ameandika kwenye ukurasa wetu wa Facebook.
King Majuto pia anakiri kutumia simu sana, ila anasema alijaribu kupunguza akashindwa.
Katika kujaribu kuacha uraibu huu, Zakayo Samsom kwenye Instagram anasema alijiwekea malengo ya kuacha kununua kifurushi cha data.
"Kidogo ilisaidia,” anasema.

Post a Comment

 
Top