0
Ndege 2 za jeshi la China zimeizua ndege moja ya kijeshi ya Marekani iliokuwa katika anga ya bahari iliopo kusini mwa China,Idara ya ulinzi nchini Marekani The Pentagon imesema.
Kisa hicho kilitokea katika anga ya kimataifa mnamo tarehe 17 mwezi Mei wakati ambapo wanamaji wa Marekani walikuwa wakipiga doria ya kawaida katika eneo hilo.
Hatahivyo,msemaji wa wizara ya maswala ya nchi za kigeni alikana madai yoyote ya kuhatarisha usalama kutoka kwa ndege hizo za China.
Mataifa kadhaa yamekuwa yakidai umiliki wa eneo hilo lililo na utajiri huko kusini mwa bahari ya China.
Image copyrightAP
Image captionNdege za kijeshi za Marekani
Hali ya wasiwasi imeongezeka hivi karibuni ,huku China na Marekani zikitupiana lawama kuhusu vitendo vyao vya kijeshi.
Afisa mmoja wa jeshi alinukuu chombo cha habari cha Associated Press ,kwamba rubani wa ndege hiyo ya Marekani alilazimika kushuka futi 200 ili kuzuia kugongana.
Baadaye siku ya Alhamisi,Hong Lei kutoka kwa wizara ya maswala ya kigeni ya China alijibu kuhusu madai hayoakisema hayakuwa ya ukweli.

Post a Comment

 
Top