0
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Staffan de Mistura anatarajiwa kukutana na waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi kujadiliana kuhusu juhudi za kunusuru kuvunjika kwa mkataba wa amani nchin Syria.
Bwana De Mistura anataka Urusi na Marekani ambazo zinaunga mkono makundi pinzani nchini humo kushirikiana ili kurejesha makubaliano waliopata mnamo mwezi Februari.
Washington imelaumu Moscow kwa kushindwa kuwazuia wanajeshi wa Syria waliopo mjini Aleppo.
Image copyrightReuters
Image captionBashar Al Assad
Lakini Moscow inasema kuwa mashambulizi ya angani katika eneo hilo yamewalenga magaidi.
Zaidi ya watu 250 wamefariki mjini Aleppo katika siku 10 zilizopita wengi wao wakiwa raia,wanaharakati wamesema.
Thuluthi mbili ya vifo hivyo vimekuwa katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi mashariki mwa mji huo ikiwemo 50 katika shambulio la angani katika hospitali ambayo Marekani inasema ni ya makusudi.
Image copyrightRIA Novosti
Image captionSergei Lavrov
Siku ya Jumanne ,waasi walirusha makombora ya roketi katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali mjini Aleppo na kusaabisha vifo vya raia 4.

Post a Comment

 
Top