Tume ya haki za kibinaadamu nchini Afrika Kusini imetakiwa kuchunguza tamko la ubaguzi wa rangi lililochapishwa na Matthew Theunissen ambalo limezua hisia kali katika mitandao ya kijamii.
Hatua hiyo inajiri baada ya tamko la bw Theunissen kuhusu hatua ya waziri wa michezo Fikile Mbalula kupiga marufuku mashiriksho ya michezo kuwania kushiriki katika michuano ya kimataifa kutokana na idadi ndogo ya wachezaji weusi katika timu.
Raga,Kriketi na riadha zimeathiriwa.
Bw Theunissen:Kwa hivyo hakuna michezo Afrika Kusini.
Baadaye alitumia matamshi ya kibaguzi na matusi kuikosoa serikali.
Chapisho hilo limevutia shutuma kali kutoka kwa raia weusi na wazungu nchini Afrika Kusini.
Taifa hilo kwa sasa linaangalia ubaguzi wa rangi kama adhabu kubwa
Post a Comment