0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji, Charles Mwijage

SERIKALI imesema uwekezaji inaoulenga hasa katika ngazi za vijijini mpaka wilayani ni ujenzi wa viwanda vidogo na vya kati. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema hilo ndilo tabaka linalotoa ajira kwa wingi lakini tabaka linaloweza kusambaa kwa urahisi kutoka mjini hadi vijijini.
“Mafanikio ya jukumu hili yanahitaji ushirikiano mkubwa kuanzia ngazi ya kijiji mpaka mkoa,” alisema Mwijage akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Midimu (CCM). Katika swali lake, Midimu alitaka kufahamu serikali ina mpango gani wa kujenga viwanda vya kusindika mazao katika mkoa wa Simiyu.
Mwijage alisema moja ya vipaumbele vya serikali hadi mwaka 2020 ni kuhimiza wawekezaji kujenga viwanda vinavyotumia malighafi za ndani hususan katika sekta ya kilimo na maliasili.
Alisema viwanda hivyo ni vile vinavyozingatia ajira kwa wingi na vile vinachochea ujenzi wa viwanda vingine, na sasa serikali inaendelea kuhamasisha uwekezaji katika maeneo hayo.

Post a Comment

 
Top