Taifa la Tanzania limeorodheshwa la mwisho Afrika Mashariki katika orodha mpya ya shirikisho la soka duniani Fifa.
Tanzania imeorodheshwa katika nafasi 129 duniani huku ikishika mkia miongoni mwa mataifa ya Afrika Kusini.
Taifa linaloongoza katika eneo hili la Afrika ni Uganda ikiwa katika nafasi ya 72,Rwanda katika nafasi ya 87,Kenya katika nafasi ya 116 na Burundi katika nafasi ya 122.
Kwa jumla Argentina bado inaendelea kuongoza katika orodha hiyo ikifuatiwa na Ubelgiji na baadaye Chile katika nafasi ya tatu.
Mabingwa wa kombe la dunia Ujerumani wanashikilia nafasi ya 5 huku Uhispania na Brazil zikifuata katika nafasi ya tano na sita mtawalia
Post a Comment