0
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon, ametaka pande zinazo zozana nchini Syria kusuluhisha tofuati zao na kushirikiana katika kuidhinisha amani.
Ameonya pande hizo kwamba zina hatarisha kuangamia kwa watu na miundo mbinu ya nchi hiyo.
Katika mazungumzo pekee na BBC Geneva, Ban amesema ghasia zinazoendelea Syria zinatia wasiwasi mkubwa.
Katibu mkuu huyo alizungumza siku mbili tu baada ya awamu ya tatu ya mazungumzo ya amani Syria kumalizika Geneva pasi hatua kupigwa.
Image copyrightAP
Image captionKatibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon
Ban Ki Moon alisisitiza ukaguzi wa maafisa wake wa juu wa kutoa misaada:'hali nchini Syria ni mbaya sana'.
Machafuko yanayoendelea, Ban amesema, yanatishia uwepo wa watu wa taifa hilo.
Akiuliza swali alilolilenga kwa pande zinazo zozana Syria, Ban alikumbusha kwamba vita nchini humo vimeendelea kwa mwaka wa sita sasa na kuuliza 'vitaendelea hadi lini?'
Alitoa wito kwa pande hizo kufikiria zaidi ya misimamo binafsi na kugusia kushindwa kwa Ulaya kukabiliana na janga la wakimbizi, ameongeza kuwa vita vya Syria vina athari za kutia wasiwasi kote duniani katika kulinda haki za binaadamu na maisha ya watu.

Post a Comment

 
Top