0
Umoja wa mataifa unasema kuwa huenda wahamiaji wapatao 700 wanahofiwa kufariki katika kipindi cha siku tatau zilizopita katika bahari ya Mediterranean.
Msemaji wa Shirika la umoja wa mataifa linalowahudumia wakimbizi, Carlotta Sami, amesema kuwa mashua kadhaa yalizama katika maeneo ya kusini mwa Italia Jumatano usiku ikiwa na wahamiaji hao.
Wahamiaji waliokololewa juma lililopita kutoka katika boti moja kwenye bahari ya Mediterranea, wamewaambia wafanyikazi wa makundi ya uokoaji kuwa, waliona chombo kimoja cha baharini kilichojaa wakimbizi kikizama.
Image copyrightAFP
Image captionJuma lililopita pekee, zaidi ya watu 13,000 wameokolewa katika bahari ya Mediterranean.
Shirika moja la uokoaji la Save the Children, limeiambia BBC kuwa manusura hao walisema kuwa walingoa nanga katika msafara wa maboti matatu Jumatano usiku kutokea Libya.
Maafisa wa Polisi wa Italia wanasema waliwahoji wahamiaji hao waliofika mjini Sicily hapo Jana Jumamosi.
Juma lililopita pekee, zaidi ya watu 13,000 wameokolewa katika bahari ya Mediterranean

Post a Comment

 
Top