Mahakama nchini Kenya imetoa uamuzi unaoruhusu majina ya baba wazazi wa watoto wanaozaliwa nje ya ndoa kujumuishwa kwenye vyeti vya kuzaliwa vya watoto hao bila wanaume hao kuombwa idhini.
Akitoa hukumu hiyo jaji Mumbi Ngugi alisema kuwawatoto wanaozaliwa nje ya ndoa wanakumbwa na ubaguzi.
Alisema kuwa kila mtoto ana haki ya jina la babake kuandikwa kwenye cheti chake cha kuzaliwa.
Ruhusa ya baba haitahitajika jinsi imekuwa hadi sasa, ambapo unapata kuwa vyeti vingi vina herufi Xs kwenye nafasi inayostahili kujazwa jina la baba.
Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na mwanamke ambaye hajaoelewa, ambaye alitaka jina la baba yao kujumuishwa kwenye vyeti vya watoto wake, akidai kuwa wanabaguliwa kwa misingi ya urithi.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.