Wakili wa kiongozi wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Moise Katumbi, amesema kuwa kiongozi huyo amepelekwa Afrika Kusini kwa matibabu.
Wakili huyo, Georges Kapiamba amesema kuwa Bwana Katumbi amelazwa hospitalini tangu Ijumaa, wakati ambapo polisi walipomtifulia moshi wakati wa maandamano.
Analaumiwa na Serikali kwa kuwakodisha mamluki kutoka nje ya nchi kwa lengo la kupindua Serikali.
Lakini Bwana Katumbi amekanusha mashtaka na kusema kuwa yana lengo la kuvuruga kampeni zake za kutaka kumrithi Rais Joseph Kabila katika Uchaguzi unaotarajiwa kufanywa Novemba.
Serikali ilisema Bwana Katumbi aliamua kwenda Afrika Kusini kwa matibabu, siku moja baada ya waranti ya kumtia mbaroni kutolewa.
Rais Kabila, ambaye ametawala tangu mwaka 2001 anazuiwa kikatiba kugombea muhula mwingine
Post a Comment