Volkano inaendelea kulipuka katikati mwa Costa Rica, huku ikirusha angani moshi na majivu kwa umbali wa zaidi ya kilomita tatu.
Mamia ya watu wameenda hospitali wakilalamikia shida ya kupumua na matatizo ya ngozi.
Shule kadhaa nchini humo zimefungwa na safari za ndege kusitishwa au kubadilishiwa njia zinakofuata.
Watu katika mji Mkuu wa San Jose, zaidi ya kilomita 30 kutoka Volcano hiyo ya Turrialba, walisema kuwa majivu yamesambaa kwenye mijengo na magari na kuna harufu kali ya kemikali ya Sulphur.
Shirika la kupambana na maswala ya hatari nchini imewatahadharisha watu kufunika mapua yao na vitambaa vya kujikinga na kuhakikisha wamevaa nguo za kubana ili kukinga mapafu na ngozi zao.
Post a Comment