0
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anasema hataki "kuombwa msamaha na yoyote" baada ya waziri mkuu wa Uingereza David Cameron kuitaja nchi yake kama "taifa lenye ufisadi mkubwa".
Akizunhgumza katika hafla ya kupambana ufisadi London, Buhari amesema zaidi angependa kurudishiwa mali yote iliyoibiwa Nigeria inayozuiwa katika mabenki ya Uingereza.
Cameron alitoa tamko hilo katika mazungumzo na Malkia Elizabeth.
Ameandaa mkutano wa kimataifa wa kupambana na ufisadi Alhamisi.
Image copyrightAFP
Hotuba ya Buhari katika mkutano huo katika makao ya jumuiya madola London inafuata taarifa iliyotolewa kutoka ofisi yake inayosema kwamba "ameshutushwa naku aibishwa" na kauli ya Cameron.
Alipoulizwa iwapo Nigeria ni "taifa lenye ufisadi mkubwa", Buhari alijibu: "ndio".
Nigeria imeorodheshwa 136 kati ya nchi 167 katika faharasha ya shirika la Transparency International mwaka 2015.
Katika hotuba yake, kiongozi huyo wa Nigeria ametaja ufisadi kama jinamizi linalotishia usalama wa mataifa "na halina tofuati katika matifa yalioendelea na yanayoendelea".
Amesema rushwa Nigeria ni janga na serikali yake inawajibika kupambana nalo.

Post a Comment

 
Top