0
Bofya hapa kwa habari za karibuni zaidi
17:47 Ni wakati wa mapumziko:
  • Everton 0-0 Southampton
  • Man Utd 1-0 Aston Villa
  • Newcastle 1-0 Swansea
  • West Brom 0-1 Watford
17:45 Man Utd 0-1 Aston Villa
Villa wanapata nafasi baada ya Jordan Ayew kumchenga Chris Smalling eneo la hatari. Lakini anasita kidogo na Morgan Schneiderlin anamzuia.
17:41 West Brom 0-1 Watford
West Brom wanajaribu kujikwamua. Saido Berhino anapiga kombora lakini linatoka nje. Stephane Sessegnon naye anajaribu lakini mpira wake unakosa goli pembamba.

17:40 BAOOOOO! Newcastle 1-0 Swansea

Kupitia kona, Jamaal Lascelles anafungia Newcastle.
17:39 Everton 0-0 Southampton
Pigo kwa Southampton. Nahodha wao Mreno Jose Fonte anaumia. Mjapani Maya Yoshida anajiandaa kuingia nafasi yake.
17:36 Newcastle 0-0 Swansea
Newcastle wanaendelea kushambulia lakini bahati yao bado haijasimama.

17:31 BAOOOOO! Man Utd 1-0 Aston Villa

Marcus Rashford anawaweka United kifua mbele baada ya kupokea pasi kutoka kwa Antonio Valencia. Sasa amefunga mabao saba katika mechi 12 alizowachezea United.
Image copyrightGETTY
17:31: Man Utd 0-0 Aston Villa
Manchester United wamepata kona tisa kufikia sasa. Lakini hawajaweza kumtatiza kipa wa Aston Villa Brad Guzan

17:27 BAAAOOOO! West Brom 0-1 Watford

Uwanjani Hawthorns, Ben Watson anatikisa wavu.
17:26 Newcastle 0-0 Swansea
Gylfi Sigurdsson anateleza akipiga frikiki. Mkwaju wake unapaa juu na kutoka nje.
17:23 Everton 0-0 Southampton
Southampton wameanza kudhibiti mpira. Wamepata naafsi mbili nzuri. Mpira wa Jordie Clasie umepaa juu ya mwamba wa goli. Kombora la Shane Long slashes pia limekosa wavu.
17:18 Man Utd 0-0 Aston Villa
Image copyrightPA
Wayne Rooney anatuma krosi lakini mpira wa kichwa wa Fellaini unatoka nje.
17:15 Everton 0-0 Southampton
Southampton wanashambulia. Mara ya kwanza kupitia Cuco Martina na pili kupitia Mkenya Victor Wanyama. Lakini hawamtatizi kipa mwenyeji Joel Robles.
17:14 Newcastle 0-0 Swansea
Newcastle wanakaribia kufunga. Vurnon Anita anatuma krosi kutoka upande wa kulia lakini kipa wa Swansea anazinduka upesi na kuondoa mpira huo eneo la hatari. Anita anarejea tena na kumwandalia Andros Townsend lakini mpira wa Townsend unatua mikononi mwa Fabianski.
17:13 West Brom 0-0 Watford
Uwanjani Hawthorns, mambo yametulia. Hakuna aliyeona lango la mwenzake.
17:10 Man Utd 0-0 Aston Villa
Leandro Bacuna anatumia kichwa kuwazuia Mata na Memphis kufunga huku United wakiendelea kushambulia.
17:06 Leicester City ambao wanaongoza kwenye jedwali watashuka dimbani kesho dhidi ya West Ham.
17:05 Manchester United wameanza kwa kudhibiti mpira. Mambo bado ni 0-0.
17:00 Wachezaji mechi ya Manchester United na Aston Villa
Man UtdAston Villa
De GeaGuzan
A ValenciaHutton
SmallingClark
BlindLescott
RojoCissokho
FellainiBacuna
SchneiderlinWestwood
MataSinclair
RooneyGueye
DepayRichardson
RashfordJ Ayew
BenchiBenchi
MartialRichards
YoungSánchez
RomeroGil
McNairBunn
LingardLyden
DarmianGestede
Fosu-MensahGrealish
17:00 Mechi nne zinaanza:
  • Everton v Southampton
  • Man Utd v Aston Villa
  • Newcastle v Swansea
  • West Brom v Watford
RashfordImage copyrightAP
Image captionRashford anashirikiana na Rooney kwenye mashambulizi
16:50 Hujambo. Karibu kwa taarifa za moja kwa moja za mechi za Ligi Kuu ya Uingereza. Mechi sita zinachezwa leo. Tayari mechi ya kwanza imekamilika, Sunderland wakiwapokeza Norwich City kichapo cha 3-0. Manchester United, Manchester City na Chelsea pia watashuka dimbani.
  • Norwich 0-3 Sunderland
  • Everton v Southampton 17:00
  • Man Utd v Aston Villa 17:00
  • Newcastle v Swansea 17:00
  • West Brom v Watford 17:00
  • Chelsea v Man City 19:30

Post a Comment

 
Top