Mikheil Saakashvili ambaye ni rais wa zamani wa Georgia na pia gavana wa zamani wa jimbo nchini Ukrain amevuka na kuingia nchini Ukrain aisaidiwa na mamia ya wafuasi wake.
Bwana Saakashvili alisema kuwa alisukumwa bila kutarajia kwenye mpaka na umati wa watu waliokuwa wamekasirika kuwa mpaka ulikuwa umefungwa.
"Walitusukuma na kutebeba hadi nchini Ukarain," alesema Saakashvili.
Maafisa nchini Ukrain wanasema kuwa aliiangia nchini humo kinyume na sheria na walinzi 15 na mpaka walijeruhiwa.
Kulikuwa na mivurutano kwenye mpaka kati ya wafuasi wa bwana Saakashvili na maafisa wa mpaka.
Bwana Saakashvili ambaye awali alikuwa ni raia wa Georgia na kisha raia wa Ukrain kwa sasa hana uraia wa nchi yoyote baada ya uraia wake wa Ukrain kufutwa na mshirika wake wa zamani raid Petro Poroshenko.
Pia anatakiwa nchini Georgia kwa kesi zinazohusu uhalifu ambazo anadai kuwa zimechochewa kisiasa.
Mapema Jumapili treni yake ilizuiwa katika kituo huko Przemysl nchini Poland baada ya walinzi wa Ukrain kumzuia kuingia.
Bwana Saakashivili alijiunga na wafuasi wake kadha akiwemo waziri mkuu wa zamani wa Ukrain na kiongozi wa sasa wa upinzani Yulia Tymoshenko.
Mwaka 2015 aliteuliwa gavana wa Odessa na Bw. Poroshenko lakini wawili hao walitofautiana mwezi Novemba mwaka uliopita baada ya Bw Saakashvili kumlaumu rais wa kuzuia jitihada za kumaliza ufisadi.
Lakini alipokuwa akikubali uaria wa Ukrain alisalimisha uraia wa Georgia.
Akiwa nchini Ukrain anaweza kukamatwa na kurudishwa nchini Geogia ambapo atafunguliwa mashtaka.
Post a Comment