0
Oparesheni ya kiusalama inayowalenga waislamu wa Rohingya nchini Myanmar ni mfano wa mauaji ya kikabila, mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema.
Zeid Raad Al Hussein ameitaka Mynamar kusitisha oparesheni mbaya ya kijeshi katika jimbo la Rakhine.
Zaidi ya watu 300,000 waisilamu wa Rohingya, wamekimbia kwenda Bangaladesh tangu ghasia zianze mwezi uliopita.
Jeshi linasema kuwa linajibu mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa Rohingya na kukana kuwalenga raia.
Ghasia hizo zilianza tarehe 25 mwezi Agosti wakati wapiganaji wa Rohingya walishambulia vituo vituo vya polisi kaskazini mwa Rakhine na kuwaua maafisa 12 wa ulinzi.
Rohingya ambao wameikimbia Myanmar tangu wakati huo, wanasema kuwa wanajeshi walijibu vikali kwa kuchoma vijiji na kuwashambulia raia kwa minajili ya kuwafukuza.
Rohinga ambayo ni jamii ndogo ya waislamu wasio na utaifa wamekumbwa na mauaji kwa muda mrefu nchini Myanmar ambayo inasema kuwa wao ni wahamiaji haramu.


Post a Comment

 
Top