Meneja wa Manchester Pep Guardiola
amesema hakukuwa na uwezekano wowote kwamba Manchester City
wangemuongeza Raheem Sterling kwenye mkataba wa kumnunua mshambuliaji wa
Arsenal Alexis Sanchez.
Arsenal walikuwa wameafikiana na City
uhamisho wa £60m kwa Sanchez, 28, lakini hilo lilitegemea kufanikiwa kwa
Gunners kumchukua Thomas Lemar.Lemar hata hivyo aliamua kusalia Monaco.
Guardiola amesema Gunners walitaka Sterling, 22, kama sehemu ya mkataba wa kumuuza Sanchez.
"Walizungumza nami. Lakini nikasema haiwezekani," amesema Guardiola.
"Tulisema tulitaka kuwalipa pesa taslimu kwa ajili ya Alexis. Walikubali lakini hawangeweza kumnunua mchezaji waliyemtaka, kwa hivyo alisalia Arsenal.Sterling amechezea City mechi tatu msimu huu na kufunga mabao mawili.
Alifukuzwa uwanjani kwa kusherehekea sana bao la dakika za mwisho la ushindi dhidi ya Bournemouth kabla ya mapumziko ya kimataifa.
Alichezea England mechi mbili wakati wa mapumziko ya kimataifa.
Post a Comment