Barcelona wapo tayari kutoa pauni milioni 80 kumtaka Philippe Coutinho, 25, kutoka Liverpool. (Sunday Mirror)
Mshambuliaji
wa Barcelona, Lionel Messi, 30, ameiambia klabu yake kumsajili
mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala, 23. (Don Balon)
Meneja wa
Liverpool Jurgen Klopp amesema Coutinho "ametulia" Liverpool baada ya
klabu hiyo kuzungumza naye kufuatia hatua ya Barcelona kumtaka. (ESPN
FC)
Liverpool hatimaye wamefikia makubaliano na RB Leipzig ya pauni milioni 75 ili kumsajili Naby Keita. (Winner Sports)
Meneja
wa Arsenal amekanusha taarifa kuwa Alexis Sanchez, 28, anakaribia
kuhamia Paris Saint-Germain kwa pauni milioni 70. (Standard)
Alexis
Sanchez anataka mshahara wa pauni 500,000 kwa wiki kutoka Paris
Saint-Germain, huku akikaribia kuhamia Paris. (The Mirror)
Liverpool na Arsenal wameonesha dalili za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Lucas Vasquez. (Diario Madridista)
Chelsea wanapanga kuzungumza na Arsenal kuhusiana na Alex Oxlade-Chamberlain, 23. (Sky Sports)
Chelsea
wanamfuatilia winga wa Montreal Impact Ballou Jean-Yves Talba, baada ya
Didier Drogba kuwaambia kuhusu mchezaji huyo. (Sun)
Manchester
United wana uhakika wa kumsajili kiungo wa Chelsea Nemanja Matic, 28,
baada ya kumkosa Eric Dier, 23, wa Tottenham. (Guardian)
Mipango
ya Manchester United kutaka kumsajili kiungo wa PSG, Marco Verratti, 24,
kwa pauni milioni 60 imesitishwa kwa muda baada ya PSG kusema inamtaka
Anthony Martial, 21. (Sunday Mirror)
Jose Mourinho amesema "ana
uhakika" David de Gea atabakia Manchester United msimu huu, baada ya
Real Madrid kushindwa kutumia nafasi ya kumsajili kipa huyo. (Sky
Transfer Centre)
Manchester United sasa wamemgeukia kiungo wa Bayern Munich, Arturo Vidal, wakati wakitafuta kiungo mpya. (Daily Star)
Beki wa Manchester United Matteo Darmian, 27,
amesema haendi popote licha ya taarifa kumhusisha na kurejea Italy.
(Press Association)
Real Madrid wametengeneza orodha ya
washambuliaji inayowataka, ikiwa watamkosa Kylian Mbappe. Miongoni mwao
ni Marcus Rashford wa Manchester United, Pierre Emerick-Aubameyang wa
Borussia Dortmund na Timo Werner wa RB Leipzig. (Diario Gol)
Real
Madrid watamsajili mshambuliaji wa Ajax Kasper Dolberg pamoja na
Domenico Berardi wa Sassuolo, iwapo watamkosa Kylian Mbappe. (Marca)
Real Madrid wamewaambia Monaco watawapa Karim Benzima kama sehemu ya mkataba wa kumsajili Kylian Mbappe. (The Sun)
Chelsea wamemuulizia winga wa Inter Milan Antonio Candreva, ili kuogeza ushindani Stamford Bridge. (the Sun)
Kiungo wa Manchester City Kevin de Bruyne, 26,
amesema ana matumaini klabu yake itanunua mabeki wengine kadhaa msimu
huu. (Manchester Evening News)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza
mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha
rasmi usajili bofya link hii:
http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na Jumapili njema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment