0
Waziri mkuu nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Samy Badibanga amejiuzulu kama sehemu ya makubaliano yaliyoongozwa na kanisa katoliki kumaliza mzozo wa kisiasa nchini humo, kwa mujibu wa Redio moja ya nchi hiyo, Redio Okapi.
Hii inafuatia hotuba ya hapo jana kutoka na Rais Joseph Kabila, ambapo aliwaambia wabunge kuwa atamteua waziri mkuu kutoka upinzani ndani ya saa 48 zinazokuja.
Bwana Kabila alisema kuwa atafuata tararibu zilizoafikiwa kama sehemu ya makubaliano na upinzani ambayo yanataka uchaguzi kuandaliwa kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Kumekuwa na msukosuko nchini DRC baada ya Kabila kukataa kundoka madarakani wakati muhula wake ulipokamilika mwezi Disemba.

Post a Comment

 
Top