0
Mahakama ya juu zaidi nchini Brazil imepiga marufuku migomo yote ya polisi ikisema kuwa migomo hiyo inaenda kinyume na katiba.
Katika amri hiyo mahakama ilipiga marufuku migomo yote ya polisi pamoja na ya wazima moto.
Mgomo wa polisi kati jimbo la Espirito Santo, ulisababisha ghasia mwezi Februari, huku shule zikifungwa na usafiri wa umma kusitishwa.
Migomo ya polisi si jambo la nadra nchini Brazil na siku za nyuma imezua matatizo katikaa miji mikubwa kama vile Rio na Sao Paulo pamoja na jimbo la Bahia.
Majaji walisema kuwa yeyote ambaye anafanya kazi katika idara inayohusika na usalama wa umma, hana haki ya kugoma kwa njia yoyote ile kwa sababu ana wajibu muhimu wa kulinda nchi.
Muda mfupi baada ya kutolewa amri hiyo , chama kinachowaakilisha polisi kilisema kuwa wanachana wake walikuwa wamepiga kura ya kufanya mgomo kote nchini kupinga mswada unaohusu maslahi ya polisi.
Mwezi Februari mamia ya polisi na jeshi walitumwa katika jimbo la Espirito Santo baada ya visa vya mauaji kupanda kufuatia mgomo wa polisi waliokuwa wakiomba nyongeza ya mishara.
Polisi wakiwa kwenye maandamao Februari mwaka huuHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionPolisi wakiwa kwenye maandamao Februari mwaka huu

Post a Comment

 
Top