0
Yule mwanamume wa India anaependa kuvalia mrundo wa dhahabu hadi kubandikwa jina The Gold Man ameuawa.
Mtu huyo kwa jina Datta Phuge aliwahi kununua shati mojawapo ghali zaidi duniani kwani lilikuwa la dhahabu.
Dhababu ya shati hilo inasemekana hapo 2013 ilikuwa kilo tatu 3kg na liligharimu $250,000.
Polisi wamewakamata wanaume wanne kuhusiana na mauaji ya Datta Phuge.
Tetesi ni kuwa huenda si shati lake la dhahabu wala vito na vyombo vya dhahabu anavyovaa vilivyomchongea kuawa bali wanashuku ulikuwa mzozo wa kifedha.
Phuge alikuwa akifanya biashara ya kukopesha watu fedha kwa faida na huenda alikosana na baadhi ya wateja wake.
Katika uhai wake aliwahi kuulizwa kwanini anapenda kuvalia na kujinakshi kwa dhahabu chungu nzima, jibu lake ni hili....Hiyo ndio imekuwa ndoto yangu tangu zamani, kama vile watu wengine hupenda magari ya kifahari kama vile Audi ,Mercedes, nami napendelea mng'aro wa dhahabu'' .

Post a Comment

 
Top