0


Ikulu ya White house nchini Marekani inasema kuwa utawala wa Donald Trump haujachukua msimamo rasmi kuhusu ujenzi wa makaazi ya Israel katika ardhi ya Palestina, lakini upanuzi zaidi wa makaazi hayo huenda ukaathiri mazungumzo ya amani katika eneo hilo.
Taarifa hiyo inajiri saa kadhaa baada ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuahidi kuanzisha ujenzi wa makaazi mapya ya serikali baada ya kituo cha kijeshi cha Amona kuharibiwa.

Rais wa Marekani Donald Trump
Image captionRais wa Marekani Donald Trump

Tangu kuapishwa kwa rais Donald Trump ambaye ameonekana kupendezwa na ujenzi wa makaazi hayo, Israel imetangaza mipango yake ya kujenga makaazi mapya 6000.

Post a Comment

 
Top