Wana mazingira nchini New Zealand, wanasema nyangumi wengine mia mbili na 40 wa aina ya "pilot", wamekwama katika ghuba ilioko mbali, kwenye kisiwa cha kusini cha New Zealand.
Kundi hilo jengine la nyangumi lilikwama kwenye ufukwe unaoitwa Farewell Spit, punde baada kundi la nyangumi mia moja kusaidiwa kurudi baharini maji yalipojaa.
Nyangumi mia tatu walikufa jana.
Eneo hilo la pwani la kilomita 20, lenye maji ya kina kifupi, ni gumu kwa nyangumi kuogelea.
Ingaiwa kuwa huenda nyangmi hao walisukumwa hadi ufukweni na papa baada ya alama za kung'atwa kupatikana katika mmojawapo wa nyangumi hao aliokufa.
Hathivyo haijulikani ni kwa nini nyangumi hao wanaendelea kuwasili katika ufuo huo wa kilomita 5 karibu na Golden Bay.
Wataalam wanasema kuwa nyangumi ambao hujipata ufukweni hutoa wito kwa wenzao ambao nao pia hujipata katika ufukwe.
Post a Comment