0
Raia mmoja wa Uingereza anayepigana nchini Syria alijipiga risasi na kujiua ili kuzuia kukamatwa na wapiganaji wa IS kulingana na BBC.
Ryan Lock kutoka Chichester huko West Sussex nchini Uingereza alifariki akiwa na umri wa miaka 21 mnamo mwezi Disemba wakati wa vita dhidi ya IS katika ngome yao ya Raqqa.
Alikuwa amejitolea kupigana na wapiganaji wa Kikurdi YPG.
Kundi hilo limeambia BBC kwamba uchunguzi wao umeonyesha kuwa kijana huyo alikuwa na kidonda cha risasi chini ya kidevu chake, ikimaanisha kwamba alijiua.
Duru zinaarifu kuwa wapiganaji hao walizingirwa katika kijiji cha Ja'bar na kuonyesha kutosalimu amri kabla ya kuuawa.
Baada ya miili yao kupatikana ukaguzi ulibaini kwamba mpiganaji huyo wa Uingereza alijiua ili kutoweza kukamtwa na IS.
Ripoti hiyo ilisema kuwa jeraha hilo la risasi linaonyesha kuwa bunduki hiyo ilikuwa imewekwa chini ya kidevu chake .

Post a Comment

 
Top