Mtu mmoja katika jimbo la Masachussets nchini Marekani ameshtakiwa kwa tuhuma za kutekeleza uhalifu wa chuki baada ya kumpiga teke mfanyikazi Muislamu katika uwanja wa ndege wa JFK pamoja na kumkaripia.
Robin Rhodes mwenye umri wa miaka 57 anatuhumiwa kwa kusema Trump....atawafukuza nyinyi nyote na baadaye akamzuia mwanamke huyo kutoondoka katika afisi yake.
Kushambulia na kuwazuilia watu ni miongoni mwa mashtaka ya uhalifu wa chuki ambao mtu huyo kwa sasa anakabiliwa nayo ,kulingana na hakimu wa Queens District.
Anakabiliwa na kifungo cha miaka 4 jela iwapo atapatikana na hatia.
Mfanyikazi huyo wa kampuni ya ndege ya Delta Airlines ambaye alikuwa amevaa hijab alikuwa ameketi katika afisi yake siku ya Jumatano wakati Rhodes alipodaiwa kwenda katika mlango wake na kuanza kumkaripia, kugonga mlango, kumzuia kuondoka na kumpiga teke.
Wakati mtu mwengine alipoingilia kati na kumsaidia mwanamke huyo kutoka afisini mwake, mtu huyo alidaiwa kumfuata na kupiga magoti mbele yake akiigiza maombi ya kiislamu.
''Islam na Isis, sasa Trump amewasili. Atawafurusha nyote. Unaweza kuuliza Ujerumani, Ubelgiji na Ufaransa kuhusu watu hao.utaona kilichojiri''.
Pia ameshtakiwa kwa kupiga kelele.
Post a Comment