0
Rais mteule wa Marekani Donald Trump, ametangaza kuwa atatenganisha maslahi yake ya kibiashara kabisa na majukumu yake kama rais wa Marekani.

Katika ujumbe aliotuma kwenye mtandao wake wa kijamii wa twitter, Trump amesema licha ya kuwa hashurutishwi kuchukua uamuzi huo, amedhani ni hatua muafaka ili kuzuia mgongano wa maslahi.
Bwana Trump amesema atatoa maelezo zaidi mwezi ujao akiwa na wanawe katika kikao na waandishi wa habari.

Wakati huo huo Trump amemteua afisa wa zamani za kampuni ya Gold maan sach, Steven Mnuchin kuwa waziri wake wa fedha.

Mnuchin mwenye umri wa miaka 53 aliongoza operesheni za kifedha za trump wakati wa kampeini.
Uteuzi huo hata hivyo unahitaji kuidhinishwa na bunge senate.


Bw Trump na maafisa wake wa mpito bado hawajaidhinisha uteuzi huo ambao ulitajwa na wingi kupitia uvumi.
Badala yake bw Trump alichagua kuangazia mipango yake ya kutenganisha maslahi yake ya biashara na kazi yake mpya.

Post a Comment

 
Top