Kiungo wa kati Paul Pogba na
Marouane Fellaini watakosa mechi ya kulipiza kisasi ya robo fainali
dhidi ya West Ham baada ya kuhudumia marufuku.
Mshambuliaji wa West Ham Diafra Sakho ,ambaye alifunga bao katika uwanja wa Old Trafford wikendi iliopita anauguza jeraha la kifundo cha mguu.
Anday Caroll yuko karibu kurudi katika kikosi cha kwanza baada ya kuuguza jeraha la goti huku beki Winston Reid akirudi baada ya kuhudumia marufuku.
Kiungo wa kati wa Manchester United Ander Herrera amesema kuwa itakuwa mechi ya ''kulipiza kisasi'' baada ya timu yake kufeli kuishinda West Ham wikendi iliopita.
Katika mechi nyengine Arsenal itaikaribisha West Ham katika uga wa Emirates
Post a Comment