0
Vikosi vya usalama nchini Myanmar vimesema kuwa watu 17 wameuawa wakiwemo polisi tisa, mauaji hayo yametokea katika kituo cha polisi huko katika mpaka wa nchi hiyo na Bagladesh
Afisa mmoja wa Polisi amewaambia waandishi wa habari kuwa miongoni mwao ni washambuliaji wanane ambao waliuawa wakati wa mapambano katika jimbo la Rakhine.
Imeelezwa kuwa washambuliaji wawili walikamatwa.
Shambulio hilo linadaiwa kutekelezwa na jamii ndogo ya kiislamu ya Rohingya.
Kumekuwa na mvutano mkali katika Jimbo la Rakhine kati ya jamii ya Budha na jamii ya kiislamu ya Rohingya.
Shambulio la hivi karibuni linaelezwa kuwa baya zaidi kutokea jimboni Rakhine tangu mwaka 2012.

Post a Comment

 
Top