0
Rais wa colombia Juan Manuel Santos amesema kuwa atatoa pesa kutoka katika tuzo yake ya amani ya Nobel ili kuwasaidia waathirika wa mgogoro katika nchi yake. Alipata tuzo hiyo kutokana na juhudi zake za makubaliano ya amani na kundi la kigaidi la FARC.
Santos na kiongozi wa kundi hilo Timochenko walisaini makubaliano ya amani mwezi uliopita ili kumaliza mgogoro wa zaidi ya miongo miwili.
Lakini wananchi wa Colombia walipiga kura ya hapana juu ya makubaliano hayo. Santos anatarajia kupokea zaidi ya dola mia tisa elfu kutoka kamati ya Nobel.

Post a Comment

 
Top