0
Waziri wa mambo ya ndani nchini Uganda amemtetea mkuu wa polisi nchini humo Kale Kayihura, ambaye analaumiwa kwa kukataa kufika mahakamani kujibu mashtaka yanahusu dhuluma za polisi dhidi ya wafuasi wa upinzani.
Akiongea wakati wa mkutano wa waandishi wa habari mjini Kampala, Aboubakar Jeje Odongo alisema kuwa mkuu huyo wa polisi hawezi kushtakiwa kama mtu binafsi.
Karibu mawakili wa haki za binadamu 20 wako kwenye kesi inayomuandama Jenerali Kayihura, inayuhusu dhuluma dhidi wa wafuasi wa mgombea urais aliyeshindwa Kizza Besigye.
Alikataa kufika mahakamani mapema mwezi huu akidai kuwa hajapata agizo la kumtaka afanye hivyo.
Pia alishindwa kufika mbele ya kamati ya bunge inayochunguza madai hayo.
Bwana Besigye na wafuasi wake wamekataa ushindi wa Rais Yoweri Museveni uliofanyika mwezi Februari.

Post a Comment

 
Top