0
Urusi imeanza kutumia kituo cha wanajeshi wake wa angani kilicho nchini Iran, kufanya mashambulizi ya mabomu ya angani dhidi ya wanamgambo wa kiislamu nchini Syria.
Wizara ya ulinzi nchini Urusi imesema ndege hizo zenye uwezo wa kurusha mabomu ya masafa marefu zilipaa kutoka kituo cha Hamedan Magharibi mwa Iran na kuwaua wanamgambo kadhaa.
Kufikia sasa Urusi ilikuwa imefanya mashambulizi ya angani kutoka vituo vyake nchini Syria.
Kufuatia mapinduzi ya kiislamu ya mwaka 1979 , Iran imekuwa na uhusiania mbaya na Urusi, lakini uhusiano huyo umeboreka miaka ya hivi karibuni.

Post a Comment

 
Top