0
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Prof. Joyce Ndalichako ametoa siku saba kwa vyuo vikuu vilivyopokea fedha za wanafunzi ambao hawapo vyuoni kwa mwaka wa 2015/16 kuzirejesha wizarani mara moja.
Taarifa hiyo ameitoa hii leo jijini Dar es Salaam mbele ya maafisa kutoka wizarani mwake,pamoja na kaimu mkurugenzi mtendaji wa bodi ya mikopo,na mchunguzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru na wengineo.
Jumla ya vyuo vya elimu ya juu nchini Tanzania 31 kati ya 81 ndivyo vilivyohakikiwa
Image captionJumla ya vyuo vya elimu ya juu nchini Tanzania 31 kati ya 81 ndivyo vilivyohakikiwa
Kwa mujibu wa Waziri Ndalichako, uhakiki huo umefanywa na watumishi wa bodi ya mikopo kwa kushirikiana na TAKUKURU kati ya mwezi Mei hadi Julai mwaka huu ambapo wanafunzi wanufaika wa mikopo walitakiwa kujitokeza na kuonana na jopo la uhakiki ili kutambuliwa na kuhakikiwa.
Jumla ya vyuo vya elimu ya juu nchini Tanzania 31 kati ya 81 ndivyo vilivyohakikiwa.Zoezi hilo la uhakiki limefanywa katika awamu tatu kwa kila taasisi ili kuwapa nafasi wanafunzi ambao hawakuweza kujitokeza kwa uhakiki awamu ya kwanza,kujitokeza katika awamu zilizofuata.

Post a Comment

 
Top