Matatizo ya usafiri yameikumba timu ya taifa ya kandanda ya Nigeria, Super Eagles.
Super Eagles wanatarajiwa kuwasili mjini Brazil saa 36 pekee kabla ya kipenga cha kuanza kwa mashindano ya mwaka huu ya olimipiki ya Rio.
Wamiliki wa ndege walioikodisha walikataa kuendelea na safari hadi nauli yote ya kikosi hicho itakapolipwa.
Kutokana na tofauti hiyo vijana wa Samson Siasia wanatarajiwa kuwasili Brazil saa saba usiku wa kuamkia Ijumaa..
Yamkini kikosi hicho kilipofika Atlanta kilisusia kuendelea na safari yao hadi shirikisho litakapowalipa pesa zilizosalia za nauli ya ndege.
Kampuni inayomiliki ndege hiyo ilidai kuwa pesa walizoahidiwa na wizara ya michezo ya Nigeria haikuwa imefika katika akaunti zao kama walivyoahidiwa.
Chelewa chelewa hiyo imeibua wasiwasi kwani Nigeria wanapaswa kufungwa dimba hilo dhidi ya Japan katika mji wa Manau siku ya Alhamisi.
Dawati la michezo la BBC limezungumza na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo ambao wanalalama kuwa hadi sasa hawajui timu hiyo itasafiri lini.
Nigeria, iko katika kundi B pamoja na Sweden, Colombia na Japan.
Nigeria ambao miaka 20 iliyopita iliweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kutwaa nishani ya dhahabu inapigiwa upatu kufanya vyema katika mchuano huu.
Post a Comment