Ndege moja ya kijeshi ya Urusi imetunguliwa na waasi kaskazini mwa Syria, hii ni kulingana na ripoti za maafisa wa Urusi.
Kwa mjibu wa Wizara ya Ulinzi, ndege hiyo aina ya Mi-8, ilikuwa na watu watano - wafanayikazi watatu wa ndege na maafisa wawili wa kijeshi, wakati ilipoangushwa katika jimbo la Idlib.
Msemaji wa Ikulu ya Rais wa Urusi, Kremlin, amesema kuwa watu hao wote watano wamefariki.
Ndege hiyo ilikuwa ikirudi baada ya kupeleka msaada wa kibinaadamu huko Aleppo.
Kwa mujibu wa kitengo cha habari cha Interfax cha Urusi, kimemnukuu afisa mmoja akisema haijulikani ni kundi gani lililoiangusha ndege hiyo.
Post a Comment