Msongamano mkubwa wa magari unaendelea kuathiri shughuli za kibiashara jijini Nairobi kufuatia kufungwa kwa muda kwa baadhi ya barabara saba wakati wa zaiara ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Kamanda wa kaunti ya Nairobi Japheth Koome anasema kuwa barabara ya Chiromo, kati ya Westlands na Museum Hill zitaendelea kufungwa siku nzima kwa magari yanayotoka Westland kuelekea katikati ya jiji.
Hatahivyo hatua hiyo haitaathiri magari yanayotoka katikati ya jiji kuelekea Westlands.
Baadaye,barabara ya Uhuru Highway ,Haile Selassie,barabara ya bunge na ile ya Wabera zitafungwa.
''Katika shughuli pia,huenda barabara za Kenyatta na ile ya ikulu ikafungwa'',alisema Koome.Ameongezea kuwa barabara ya Langata pia huenda ikafungwa kwa muda.
Post a Comment