WANANCHI sasa wanaweza kulipa malipo ya kodi mbalimbali za Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa kutumia Benki ya NMB. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati TRA na NMB walipokuwa wakiingia makubaliano, Mkuu wa Kitengo cha Miamala wa Benki ya NMB, Michael Mungure alisema ushirikiano huo umelenga kuwarahisishia raia ulipaji kodi.
Alisema mwananchi anaweza kulipa kodi mbalimbali za TRA popote alipo kwa kutumia simu iliyosajiliwa na huduma za kibenki kwa kutumia simu ya mkononi (NMB Mobile) na kulipa kodi anayoitaji na kama sio mteja pia anauwezo wa kulipa kodi hiyo kwenye tawi lolote la NMB nchini kote bila kujali alipo. Alisema makubaliano hayo yanaendelea kurahisisha hali ya ulipaji kodi kwani Benki ya NMB ina matawi mengi na karibu wilaya zote za Tanzania.
Mkuu wa Kitengo cha Miamala Benki ya NMB, Michael Mungure (kulia) akipeana mkono na Meneja wa Idara ya Maboresho ya Ukusanyaji na Ulipaji Kodi TRA, Ramadhan Sengati mara baada ya kuingia makubaliano Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Kwa makubaliano hayo sasa mwananchi anaweza kulipa malipo ya kodi mbalimbali za Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa kutumia mfumo wa Benki ya NMB ‘NMB Mobile’ au moja kwa moja kwenye tawi la NMB popote. Kushoto ni Meneja Huduma za Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili akishuhudia.
Alisema mtandao wa matawi ya nchi nchini ni mkubwa na imesambaa kwa asilimia 95 katika wilaya zote huku ikiwa na wateja milioni 1.3 wanaotumia mtandao wa NMB kupitia simu za mkononi ‘NMB Mobile’ jambo ambalo litawarahisishia wananchi ulipaji kodi mbalimbali za TRA. Alisema mteja wa NMB aliyejiunga atatakiwa kupiga *150*66# kisha kuchagua huduma ya ulipaji kodi kabla ya kufuata maelekezo mengine yatakayomuongoza kufanikisha malipo ya kodi anayoitaji kulipa. Imeingia ubia na TRA kulipa miamala ya kodi popote walipo. Popote alipo usiku au mchana kulipa kodi zote na ushuru anayoitaka. Sio mpya tumekuwa tukifanya kipya ni mfumo wa ulipaji sasa kutumia mtandao wetu moja kwa moja…mfumo wetu utaweza kumuunganisha mteja moja kwa moja na mfumo wa TRA na kufanya malipo yake.
Kwa upande wa TRA, Meneja wa Idara ya Maboresho ya Ukusanyaji na Ulipaji Kodi, Ramadhan Sengati alisema kwa ushirikiano huo na benki ya NMB sasa mifumo ya NMB inazungumza na mifumo ya TRA moja kwa moja bila usumbufu wowote na kumuwezesha mwananchi kulipa kodi yake popote alipo. Aidha alisema hatua hiyo inaleta unafuu kwa kutosumbuka sana kwa walipaji wa kodi mbalimbali na kusaidia kuondoa usumbufu.
Meneja Huduma za Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili akifafanua jambo wakati wa hafla ya kuingia makubaliano na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kukusanya kodi za TRA kupitia mfumo wa Benki ya NMB. Katikati ni Meneja wa Idara ya Maboresho ya Ukusanyaji na Ulipaji Kodi TRA, Ramadhan Sengati na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Miamala Benki ya NMB, Michael Mungure wakishiriki tukio hilo Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.
Alisema hatua hiyo pia ni inaleta usalama wa mtu kutozunguka na fedha mkononi bila sababu jambo ambalo si salama kwa muhusika. “…Hii itachangia kuongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi na mfumo bora wa ulipaji, kwani mteja anaweza kulipa kodi yoyote na hata ushuru na hata wa kimataifa kwa kutumia mfumo huu popote alipo,” alisema Sengati na kuongeza kuwa; “Malengo yetu ni kurahisisha ulipaji wa kodi ili kujenga maisha bora, huku ndio tunako enda hivyo tunawashauri wananchi watumie mfumo huu kulipa kodi mbalimbali za TRA.
Meneja wa Idara ya Maboresho ya Ukusanyaji na Ulipaji Kodi TRA, Ramadhan Sengati (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kuingia makubaliano na Mamlaka ya Mapato (TRA) na NMB kukusanya kodi za TRA kupitia mfumo wa kibenki wa NMB. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Miamala Benki ya NMB, Michael Mungure pamoja na Meneja Huduma za Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili (kushoto) wakishiriki tukio hilo Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na Benki ya NMB (kushoto) wakizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kuingia makubaliano kati ya TRA na Benki ya NMB kushirikiana katika ukusanyaji kodi za TRA kupitia mfumo wa kibenki wa NMB.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.
Meneja Huduma za Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili akifafanua jambo wakati wa hafla ya kuingia makubaliano na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kukusanya kodi za TRA kupitia mfumo wa Benki ya NMB. Kulia ni Meneja wa Idara ya Maboresho ya Ukusanyaji na Ulipaji Kodi TRA, Ramadhan Sengati akishiriki tukio hilo Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Kwa makubaliano hayo sasa mwananchi anaweza kulipa malipo ya kodi mbalimbali za Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa kutumia mfumo wa Benki ya NMB ‘NMB Mobile’ au moja kwa moja kwenye tawi la NMB popote.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.
Post a Comment