Polisi nchini Kenya wamemkamata mtu mmoja wanayesema alikuwa kiongozi wa genge la madaktari watatu waliokuwa wakipanga njama ya kutekeleza shambulizi la kigaidi linalofanana na lile lililotekelezwa Septemba mwaka wa 2014 kwenye maduka ya jumla ya Westgate mjini Nairobi.
Yamkini polisi wanawatuhumu watatu hao kwa kupanga shambulizi la kigaidi la kemikali za kibayolojia zenye viini vya maradhi ya kimeta (Anthrax).
Mohammed Abdi Ali anayejifunza kuwa daktari katika hospitali moja anadaiwa kuwa ni kiongozi wa kundi hilo la watatu ambao lilikuwa linapanga mashambulizi hayo.
Aidha Abdi Ali anatuhumiwa kuwashawishi wakenya kujiunga na makundi hayo yenye itikadi kali nchini Libya na Syria.
Ali anadaiwa kuwa mwanachama wa kundi la Islamic State.
Wenzake wawili walifaulu kuepuka mtego wa polisi.
Polisi hata hivyo wametoa majina yao na kuchapisha picha za Ahmed Hish na Farah Dagane, ambao sawa na Ali wanajifunza kuwa madaktari.
Post a Comment