0
Uingereza itakuwa na Waziri Mkuu mwanamke, ambaye atachukua majukumu kufikia mwezi Oktoba.
Hii ni baada ya wabunge wa chama tawala cha Conservative kuwateua wagombea wawili waliokuwa wanaongoza kukabiliana kuamua nani atakuwa kiongozi mpya.
Waziri wa mambo ya ndani Theresa May, ndiye anayepigiwa upatu sana kumrithi David Cameron kama kiongozi wa chama na waziri mkuu.
Waziri wa kawi Andrea Leadsom, ndiye mwanamke huyo mwingine.
Waziri wa Haki Michael Gove, aliyekuwa mmoja wa waliopigia debe Uingereza kujitoa Muungano wa Ulaya, alimaliza wa tatu kwenye kura ya akaondolewa.
Gove
Image captionBw Gove alimaliza wa tatu kura ya mchujo
Matokeo kamili yanatarajiwa mwezi Septemba.
Kinyang’anyiro cha sasa cha kuchagua kiongozi mpya kilianza baada ya Bw Cameron kuamua kung’atuka.
Hii ni baada ya upande wake, uliotaka Uingereza isalie EU, kushindwa kwenye kura ya maoni mwezi uliopita.

Post a Comment

 
Top