0
Tanzania kwa mara nyingine itawakilishwa na kikosi kidogo cha wanariadha katika Michezo ya Olimpiki, mwaka huu michezo hiyo ikifanyika Rio de Janeiro.
Tanzania itawakilishwa na wanariadha saba katika michezo hiyo itakayofanyika kuanzia Agosti 5 hadi 21.
Kikosi cha sasa hata hivyo kimeongezeka kidogo, kutoka kwa wanariadha sita waliowakilisha Tanzania Olimpiki jijini London 2012 ambao walikuwa sita.
Watakaowakilisha Tanzania Rio 2016 ni wanaume Fabiano Joseph, Said Makula na Alphonce Felix na mwanamke Sarah Ramadhan, wote wakishiriki mbio za Marathon.
Wengine ni waogeleaji Hilal Hilal na Magdalena Moshi wataoshindana mashindano ya kuogelea 50m na mwanajudo Andrew Mlugu.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki ya Tanzania (TOC) Filbert Bayi amenukuliwa na gazeti la Daily News la Tanzania akisema wanariadha zaidi huenda wakaongezwa katika ‘Team Tanzania’ iwapo watatimiza masharti yanayohitajika ya kufuzu kufikia siku ya mwisho ambayo ni Jumatatu.
Kwa jumla, kikosi rasmi cha Tanzania kitajumuisha watu 12, hao wengine watano wakiwa ni wakufunzi watatu Francis John (riadha), Alexander Mwaipasi (uogeleaji) na Judo Zaidi Hamis Omar.
Tabibu wa timu Nassor Matuzya na mkuu wa ujumbe Suleiman Jabir.
Waziri wa Michezo Nape Nnauye na Rais wa TOC Gulam Rashid pamoja na Bw Bayi pia watasafiri Rio kwa sababu ya nyadhifa zao

Post a Comment

 
Top