0
Maafisa nchini Japan wanasema kuwa tetemeko kubwa la ardhi limewaua takriban watu 19 na kusababisha uharibifu mkubwa.
Tatemeko hilo ambalo ni la pili kukumba kisiwa cha Kyushu ndani ya siku mbili, limesababisha kuporomoka kwa majengo, limeharibu barabara pamoja na mifumo ya maji na umeme.
Tetemeko hilo lilikuwa na nguvu ya 7.3 kwenye vipimo vya Richter.
Tetemeko hilo la ardhi, ambalo chanzo chake ni kilomita 10 chini ya ardhi karibu na mji wa Kumamoto, lilikuwa kubwa na liliathiri eneo kubwa kuliko la kwanza lililotokea katika mji huo wa Kumamoto Alhamisi usiku.Afisa wa serikali wa Kumamoto Tomoyuki Tanaka ameambiaAP kwamba idadi ya waliofariki inatarajiwa kuongezeka.
Wanajeshi 20,000 wametumwa kusaidia juhudi za uokoaji lakini jitihada za uokoaji zimetatizwa na mitetemeko mingine midogomidogo.
Waziri mkuu Shinzo Abe amekuwa na mipango ya kuzuru kisiwa cha Kyushi hii leo lakini safari hiyo imefutwa.

Post a Comment

 
Top