0
Sokwe mmoja nchini Uingereza amesherehekea umri wa miaka 40!
Amini usiamini Sokwe huyo alizaliwa mwaka wa 1975!
Salome, kama anavyojulikana sokwe huyo aliyezaliwa katika hifadhi ya Bristol Zoo Gardens ni mwerevu sana hasa ikiwa unampa chemsha bongo na kisha umpe chakula anachokipenda zaidi ,,,ndipo utajua uweledi wake.
Kama kutambua umri wake, wahudumu wa hifadhi hiyo walimuandalia dhifa kusherehekea kutimiza.
Image captionAmini usiamini Sokwe huyo alizaliwa mwaka wa 1975!
Kama sherehe zote za sikukuu ya kuzaliwa, Sokwe huyo alinunuliwa keki pipi ndizi na hata maua ya waridi.
Salome alikubali sokwe wenzake watano akiwemo mwanaye wa tatu Kukena mwenye umri wa miaka 4 kula keki hiyo.
Msimamizi wa hifadhi hiyo ya wanyama Lynsey Bugg, amemmiminia sifa kochokocho Salome.
Image captionSalome alinunuliwa keki na matunda na pipi
''Salome anawapenda sana wanawe na hata anamuheshimu sana babake watoto wake''
''ni jambo la kufurahisha sana kumuona Sokwe kama huyu akigonga miaka 40''

Post a Comment

 
Top