Viongozi wa mataifa ya Afrika Mashariki wameafikiana kutuma vikosi zaidi katika jamhuri ya Sudan Kusini.
Marais wa mataifa hayo ya ukanda wa Afrika Mashariki walikubaliana hayo baada ya mazungumzo ya faragha kandokando ya ya kikao rasmi cha viongozi wa Afrika mjini Kigali Rwanda.
Viongozi hao wa IGAD walitoa tamko hilo baada ya kikao na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon.
Kiongozi huyo wa UN alisisitiza kuna haja mataifa jirani yaingilie kati ilikuzuia taifa changa zaidi duniani Sudan Kusini kutumbukia katika lindi la uhasama na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
IGAD imependekeza wanajeshi hao wa ziada kuilipiga jeki jeshi la kulinda amani la UNMISS ambalo katika siku za hivi punde limelaumiwa kwa kushindwa kabisa kulinda maisha ya raia.
Viongozi wengine akiwemo rais wa Uganda Yoweri Museveni wamepinga pendekezo la kuwekewa vikwazo dhidi ya ununuzi wa silaha Sudan Kusini.
Mapendekezo hayo ni miongoni mwa mengine 6 ambayo yanatarajiwa kuratibiwa na umoja wa mataifa ya Ulaya AU inayoendelea mjini Kigali Rwanda.
Mkutano huo wa viongozi wa muungano wa Afrika unaanza leo Jumapili nchini Rwanda.
Uhusiano uliodhohofika na makahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC unatarajiwa kuwa kwenye ajenda.
Viongozi kadha wa AU wametoa wito kwa nchi za Afrika kujiondoa kwenye mahakama hiyo iliyoko mjini Hague Uholanzi wakisema kuwa inalenga zaidi viongozi wa Kiaafrika huku wazungu waliotenda makosa makubwa zaidi wakisamehewa.
Badala yake wanataka bara la Afrika kuwa na mahakama yake ambayo itashughulikia visa vya ukiukaji wa haki za binadamu.
Rais wa Sudan Omar al-Bashir -- ambaye kwa miaka mingi amekaidi amri ya kukamatwa ya ICC kwa tuhuma za uhalifu wa kivita uliofanyika Darfur yuko mjini Kigali baada ya Rwanda kumahidi kuwa hatakamatwa.
Post a Comment