Mshambulizi wa Ufaransa na Juventus Paul Pogba ameomba kuihama klabu hiyo ya Italia.
Magazeti ya michezo nchini Italia yamechapisha habari hiyo kama kichwa kuwa Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 23 ameomba aruhusiwe kuondoka kwani posho lake linavutia.
La Gazzetta dello Sport liliongoza na kichwa ''Pogba ameamua kuondoka Juventus''
Gazeti hilo linadai kuwa mfaransa huyo amekwisha kubaliana posho lake na Mashetani wekundu huku ikisisitiza kuwa sababu kuu iliyomfanya makamu wa mwenyekiti wa klabu hiyo bwana Ed Woodward asiandamane na timu ya Manchester united kwenda Uchina ilikuwa ni kwa sababu alikuwa ameamua kuandaa ombi rasmi la kumsajili mchezaji huyo wao wa zamani.
I Corriere dello Sport nalo linadai kuwa Pogba “anarejea Manchester United kwa kitita cha Euro milioni €125 million,”
Jarida lingine la michezo lenye makao yake huko Turin, Tuttosport nalo linasema kuwa Pogba ameomba ruhusa ya kuondoka.
Tuttosport, linasema kuwa ''Pogba atatia sahihi mkataba wa kipekee na wenye thamani ya pesa nyingi kupindukia utakaodumu kwa miaka mitano''
Wakala wake Mino Raiola amenukuliwa na jarida lingine akikanusha kuwa ameanza mazungumzo na klabu ya manchester United dukuduku zinadai kuwa ombi la kimsingi la Manchester United la Euro milioni moja (£85m) limekataliwa.
Aidha inadaiwa kuwa Woodward na Raiola wamekutana na meneja wa Juventus Beppe Marotta na kuomba kandarasi yake kwa Euro €101m lakini ombi lao likakataliwa.
Iwapo mkataba huu utafaulu, mfaransa huyo ndiye atakayekuwa mchezaji aliyegharimu kitita kikubwa zaidi cha fedha katika historia ya kandanda.
Post a Comment