0
Maafisa polisi huko Pakistan wanasema huenda mauaji ya mwanamitindo wa Pakistan aitwae Qandeel Baloch yalitokana na mwendelezo wa tabia katili nchini humo kwa watu kuawa kwa kisingizio cha kuwa eti wameiabisha familia.
Qandeel Baloch, mwenye umri wa miaka 26 alikuwa akipendelea kubandika picha zake zenye utata na kutoa tatanishi mtandaoni akisema yeye ni mwanamke huru wa kisasa lakini jamii na wanafamilia yake walikuwa wakishutumu vikali vitendo vyake.
Polisi wanasema wanamsaka mshukiwa wa mauji hayo ambae wanaamini ni kakake marehemu Bi Qandeel Baloch .
Awali Bi Baloch alikuwa ameitoroka Karachi na kukimbilia Punjab akihofia usalama wake.
Wengi nchini humo wamelaani mauji ya Bi Baloch akiwemo mtayarishi wa vipindi vya filamu Sharmeen Obaid-Chinoy.
Sharmeen Obaid-Chinoy aliyewahi kupata tuzo ya Oscar mapema mwaka huu kwa filamu yake The Price of Forgiveness, amenukuliwa kusema''Hamna mwanamke yeyote atakaejihisi yu salama hadi pale hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya watu wanaowauwa wenzao kwa kisingizio kuwa wameikosea heshima au kuidhalilisha familia'

Post a Comment

 
Top