Klabu ya Manchester United imemnunua kiungo wa kati raia wa Armenia aliyekuwa anayechezea klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani, Henrikh Mkhitaryan.
Mchezaji huyo wa umri wa miaka 27 amejiunga na United kwa bei ambayo haikufichuliwa.
Ametia saini mkataba wa miaka mine, na uwezekano wa kuongeza mwaka mwingine mmoja.
Nahodha huyo wa Armenia alikuwa mchezaji bora wa mwaka Bundesliga msimu wa 2015-16 Bundesliga na alifunga mabao 23 mashindano yote
"Henrikh ni mchezaji anayefaa timu sana na mwenye ustadi wa hali ya juu na uwezo wa kufunga,” meneja Jose Mourinho ameambia tovuti ya United.
"Nina furaha kwamba ameamua kujiunga na United.
"Ninaamini atafaa sana timu upesi kwani mtindo wake wa kucheza unawiana vyema sana na Ligi ya Premia.
“Sote twasubiri kwa hamu kuanza kufanya kazi naye.”
Post a Comment