0
Chelsea imemsajili kiungo cha kati wa mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza Leicester City N'Golo Kante.
Mkataba huo wa mchezaji huyo hata hivyo haijulikani imegharimu pesa ngapi japo wandani wa maswala ya uhamisho hukohuko Uingereza wanakisia kuwa Kante huenda ameigharimu the Blues takriban pauni milioni 30 hivi.
Mkataba huo mpya utamhakikisha Kante anasalia Stamford Bridge kwa kipindi cha miaka 5.
Kante alijiunga na Leicester mapema msimu uliopita akitokea Caen kwa mkataba uliogharimu pauni milioni 6.
Kiungo huyo wa kati alipata umaarufu mkubwa baada ya kufana katika mchuano wa Euro 2016 uliokamilika huko Ufaransa.
Kante, 25, huchezea timu ya taifa ya Ufaransa iliyoshindwa na Ureno katika fainali ya Euro2016.
Kante ni mchezaji wa pili kujiunga na Chelsea hususan baada ya Mshambulizi kutoka Ubeljiji Michy Batshuay aliyehamia Uingereza kutoka Marseille.
"Nafurahia sana kujiunga na kocha Antonio Conte , bila shaka wapo wengi wachezaji ambao wangependa kuichezea Chelsea'' alisema Kante.
Image copyrightAFP
Image captionMkataba huo mpya utamhakikisha Kante anasalia Stamford Bridge kwa kipindi cha miaka 5.
'' Tungependa kusalia na Kante ila hatukupata nafasi ya kumshawishi asalia hapa '' ilisema taarifa kutoka Leicester.
Wakati huo huo Conte alishindwa katika mechi yake ya kwanza akiwa kocha wa Chelsea.
Chelsea ilibanwa 2-0 na Rapid Vienna katika mechi ya kirafiki.
Kocha huyo alikishirikisha kikosi kamili kilichojumuisha nahodha John Terry Branislav Ivanovic, Nemanja Matic, Willian, Ruben Loftus-Cheek na Diego Costa.

Post a Comment

 
Top