0
Siku chache tu baada ya Uingereza kupiga kura ya kujiondoa kwenye muungano wa ulaya, sarafu ya nchi hiyo imeendelea kudorora mapema leo katika soko la ubadilishanaji wa fedha.
Baadhi ya masoko ya hisa katika bara la Asia yameanza kuimarika kufuatia kuporomoka kwa paundi kuanzia Ijumaa iliyopita.
Waziri wa fedha wa Uingereza, bwana George Osborne, amezihakikishia masoko ya Ulaya kuhusu matumaini ya siku zijazo kufuatia kura hiyo ya kujitenga.
Soko la ubadilishanji wa fedha limefunguliwa leo likiwa asilimia 0.8% chini ya kiwango kilichoshuhudiwa ijumaa.
Kigezo cha Soko la hisa la FTSE lilifunguliwa leo likiwa na pointi 6,092.19.
Image copyrightBBC CHINESE
Image captionBaadhi ya masoko ya hisa katika bara la Asia yameanza kuimarika kufuatia kuporomoka kwa paundi kuanzia Ijumaa iliyopita.
Pauni ya Uingereza ilibadilishwa na dola $1.3463, za marekani ikiwa ni asilimia 2% chini ya kiwango cha Ijumaa.
Dhidi ya sarafu ya Ulaya Euro inabadilishwa na €1.2170,ikiwa ni asilimia 1.2% chini ya kiwango cha ijumaa.
Waziri wa fedha bwana Osborne amesema kuwa uchumi wa Uingereza utalazimika kujifunga kibwebwe kwani waingereza watalazimika kusubiri kwa muda kuteuliwa kwa waziri mkuu mpya atakayetoa mwelekeo mwafaka wa taifa.
Huko Asia , serikali zimekuwa zikisaidia soko la ubadilishanaji wa fedha zisiporomoke zaidi na kuathiri vibaya uchumi wa eneo hilo.

Post a Comment

 
Top