Rais Magufuli ametangaza baraza
jipya la mawaziri huku kukiwa na mabadiliko kidogo ambapo amewaondoa
mawaziri wanne waliokuemo katika baraza la awali.
Akiwa na
takriban miaka miwili ya uongozi amesema amefanya mabadiliko hayo
kutokana na kuwepo na nafasi za wazi ambazo zinahitajika kujazwa.Mawaziri walioachwa ni aliyekuwa Waziri wa Mali asili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na nafasi yake kuchukuliwa na Hamis Kigwangwala aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Afya.
Mwingine aliyeachwa ni aliyekuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Katavi, Mhandisi Issack Kamwele aliyekuwa naibu waziri wa wizara hiyo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Juliana Shonza.
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani naye ametupwa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga.
Hili ndilo baraza jipya la mawaziri kama lilivyotangazwa na rais Magufuli:
- 1.Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
- 2.Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
II. Naibu Waziri - Joseph Sinkamba Kandege
III. Naibu Wazri - George Joseph Kakunda
- 3.Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
II. Naibu Waziri - Kangi Alphaxard Lugola
- 4.Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu.
II. Naibu Waziri - Anthony Peter Mavunde (Kazi, Vijana na Ajira)
III. Naibu Waziri - Stella Alex Ikupa (Walemavu)
- 5.Wizara ya Kilimo.
II. Naibu Waziri - Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa
.6.Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
I. Waziri - Luhaga Joelson Mpina
II. Naibu Waziri - Abdallah Hamis Ulega
- 7.Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
II. Naibu Waziri - Mhandisi Atashasta Justus Nditiye
III. Naibu Waziri - Elias John Kwandikwa
- 8.Wizara ya Fedha na Mipango.
II. Naibu Waziri - Dkt. Ashatu Kijaji
- 9.Wizara ya Nishati.
II. Naibu Waziri - Subira Hamis Mgalu
- 10. Wizara ya Madini.
II. Naibu Waziri - Stanslaus Haroon Nyongo
- 11. Wizara ya Katiba na Sheria.
Kabudi.
- 12. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
II. Naibu Waziri - Dkt. Susan Alphonce Kolimba
- 13. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga (JKT).
- 14. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
II. Naibu Waziri - Mhandisi Hamad Yusuf Masauni
- 15. Wizara ya Maliasili na Utalii.
II. Naibu Waziri - Josephat Ngailonga Hasunga
- 16. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
II. Naibu Waziri - Angelina Sylivester Mabula
- 17. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
II. Naibu Waziri - Mhandisi Stella Martin Manyanya
- 18. Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
II. Naibu Waziri - William Tate Ole Nasha
- 19. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
II. Naibu Waziri - Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile
- 20. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
II. Naibu Waziri - Juliana Daniel Shonza
- 21. Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
II. Naibu Waziri - Jumaa Hamidu Aweso
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Stephen Kagaigai kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Stephen Kagaigai alikuwa Kaimu Karani wa Baraza la Mawaziri.
Bw. Stephen Kagaigai anachukua nafasi ya Dkt. Thomas D. Kashilila ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Wateule wote wataapishwa Jumatatu tarehe 09 Oktoba, 2017 saa 3:30 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Post a Comment