Kamanda mmoja mkuu nchini Afghanistan amethibitisha kuwa kiongozi mkuu wa wapiganaji wa kundi la Taliban, Mullah Akhtar Mansour, ameuwawa.
Mullah Abdul Rauf, ambaye majuzi alipatana tena na Mansour, baada ya kukosana aliponyimwa nafasi ya kuliongoza kundi hilo la wapiganaji, ameliambia shirika la Associated Press kuwa, Mansour aliuwawa siku ya Ijumaa kwa shambulio lililotekelezwa na Marekani mpakani mwa Afghanistan na Pakistan.
Inasemekana kuwa Rais Barack Obama aliidhinisha shambulio hilo mapema.
Serikali ya Afghan na Pakistani, zinasema kuwa hazikufahamishwa kuhusiana na shambulio hilo.
Post a Comment